GET /api/v0.1/hansard/entries/372953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 372953,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/372953/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Asante sana mhe. Spika. Nilikuwa nafikiria kwamba ni jamii ya Wameru tu imeumia. Hiki ni kitu cha kushitua sana. Ukweli wa mambo ni kwamba, mwaka wa 2018 hakuna Mheshimiwa atarudi hapa. Ikiendelea vile ilivyo, hata Rais wetu, Uhuru Kenyatta, hapati kura. Ni kwa nini? Juzi nilisikia sauti kwa kipasa sauti ikisema, “Mhe. Rais, karibu Rais wetu mpendwa”. Nikashituka na nikajiuliza: “Kwani Uhuru amekuja kwangu bila kunijulisha?” Mhe. Spika, kama nitakuita Rais, Uhuru Muigai Kenyatta akija kwangu, nitamwita nani? Ninaomba, kama inawezekana, kwa sababu Bunge ndio ngao ya nchi yetu, hayo mamlaka ya gavana ni kama side mirror. Tutasema tuendeshe gari bila side mirror? Kwa nini ninasema hivyo? Ukiangalia zile pesa ambazo wamepewa, ni kama kuchukuwa mtoto mdogo na umshindilie ugali na maharagwe, hiyo ni kumpasua. Hizo pesa ni shida. Huko kwetu Meru, ukikutana na gavana, mtasimamisha magari kwa muda wa masaa mawili mpaka apite. Tukiuliza ni nani anakuja, tunambiwa ni gavana! Bw. Spika tuna taabu ya kutosha."
}