GET /api/v0.1/hansard/entries/372968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 372968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/372968/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Member",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika shida kubwa ni kwamba Bunge hili halijatengeneza sheria nzuri za kuelekeza magavana katika kazi zao. Vitu vingi vinavyofanywa katika makaunti vinafanywa kiholela tu. Hakuna sheria ya kimsingi ya kuwaelekeza magavana katika kazi zao. Tazama mambo ya barabara. Kuna sheria inayoitwa Kenya Roads Act. Hakuna sheria nyingine. Hii ndio sheria inayoelekeza jinsi mambo ya barabara yanafaa kufanywa. Bunge hili halijapitisha sheria nyingine. Tunaomba kwamba magavana na hata Mawaziri wafuate hii sheria. Hapana sheria ambayo inamwidhinisha Waziri wa Fedha kupeleka pesa kule kwenye kaunti. Hatujaunda sheria bado ya kusema kwamba pesa hasa zile za KERRA zipelekwa kwenye kaunti. Sheria iliyoko inasema kwamba pesa za KERRA zitapelekwa kwenye maeneo bunge. Hilo halifanyiki sasa! Ndiposa tunasema kwamba magavana na Mawaziri wafuate sheria. Iwapo hawatafuata sheria basi waende nyumbani na tutafute wale watu wanaojua kufuata sheria."
}