GET /api/v0.1/hansard/entries/373577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 373577,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/373577/?format=api",
    "text_counter": 33,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "July 17, 2013 PARLIAMENTARY DEBATES 4 Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Vile vile, namwunga mkono mwenyekiti wa kamati hii ya kilimo kwa pendekezo lake kwamba tupunguze kutoka siku 14 hadi siku tano muda wa uchapishaji wa Mswada huu. Hata hivyo mimi naomba kwamba huu usiwe ndio mtindo. Mambo ya kilimo hayataki kusogezewa muda. Kila kinachopitishwa na Bunge hili sharti kichukuliwe kwa uzito na kitekelezwe kwa wakati unaofaa na kwa manufaa ya wananchi wetu. Kule pwani kuna shirika linalojihusisha na nazi. Shirika hili limebaki nyuma kwa sababu ya kukosa mwelekeo na wafadhili wa kutosha. Naomba Wabunge wakubali tuwapunguzie wanakamati hawa hizi siku wanazotaka lakini haya mambo yatekelezwe kwa haraka kwa manufaa ya wananchi. Naunga mkono."
}