GET /api/v0.1/hansard/entries/37387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 37387,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/37387/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ningependa kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri. Waziri anajua kwamba ikiwa Serikali ya Kenya itaagiza mahindi ya muundo au mtindo huu wa kisayansi--- Je, ana habari kwamba itaingilia bei ya mahindi ambayo yanazalishwa hapa Kenya, na wakulima ambao wanajitokeza asubuhi mapema na kutoa jasho jembamba wakikuza mahindi ambayo wanategemea kuwapeleka watoto wao shule na kuwalisha? Kwa namna yoyote bei itashuka kwa sababu inasemekana kwamba bei ya mahindi ya kisayansi ni ya chini kuliko ya mahindi yanayozalishwa hapa Kenya! Vile vile ufafanuzi ninaotaka kutoka kwa Waziri ni kwamba utafiti ambao umefanywa unaonyesha kwamba mahindi haya yanaleta ugonjwa wa saratani, hasa sana saratani ya sehemu za siri au nyeti. Sijui kama Waziri ana habari kwamba hii itafanya idadi ya Wakenya kupungua kwa kiwango kikubwa sana; saratani ya sehemu za siri itadhuru sehemu za uzazi za akina mama."
}