GET /api/v0.1/hansard/entries/375101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 375101,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375101/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuishi Dandora. Naamini kuna umuhimu wa kubuni kiwanda ambacho kitaweza kugeuza uchafu ule uwe mbolea, ama zile karatasi zitengenezwe upya kwa manufaa ya nchi. Tukibuni hivi viwanda tutakuwa tumeongeza thamani katika nchi kwa sababu tutabuni ajira kwa vijana wetu. Itakuwa bora tuwe na viwanda hivyo katika Muthurwa, Dandora, na Kibera. Vile vile tuvibuni viwanda hivyo huko Mombasa, Malindi na Kisumu.Ukiteremka Malindi ni vile vile; ni sehemu zote za nchi. Nafikiri Kisumu hata itaongoza kwa sababu--- Haya! Wacha hivyo hivyo. Mheshimiwa Kinara, kwa hakika Hoja hii imekuja kwa wakati unaofaa na ni muhimu tukaweze kuitekeleza kwa haraka ama tuipitishe kwa haraka ili viwanda vibuniwe kwa wingi ili vijana wetu wazidi kupata ajira."
}