GET /api/v0.1/hansard/entries/375229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 375229,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375229/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuiunga mkono hoja hii iliyoletwa na mhe. Francis Kige Njenga. Tunafahamu kwamba tunayo ruwaza ya 2030. Hivyo basi ili tuweze kufikia ruwaza hii ni lazima tuangalie taasisi zetu za kuwapa ujuzi watoto wetu. Serikali imengâangâana kutuletea taasisi hizi vijijini. Taasisi hizi ni nyingi lakini ajabu ni kwamba vijana wetu bado hawajapata mafunzo. Hii ni kwa sababu ya umaskini. Wazazi wengi wanashindwa kulipa karo. Serikali hivi punde ilipunguza karo katika taasisi hizi za vijijini lakini bado katika takwimu zile zinaonekana, watoto wanaokwenda kupata masomo ni wachache sana na hii yote ni kwa sababu ya umasikini. Wakati tutakuwa na mfumo kama huu ambao utawezesha vijana wetu kuweza kupata pesa ambazo zitawasimamia katika kuweza kupata ujuzi, basi tutaweza kuwaboresha na kuwajenga. Tunajua ya kwamba Serikali yetu ya Jubilee, katika kuongeza kazi, njia moja ambayo wamefikiria ni Jua Kali. Wakati tunataka kuboresha Jua Kali lazima tuangalie tutaiboresha kwa njia gani. Njia moja ni kuweza kuwapa tauluma vijana wetu."
}