GET /api/v0.1/hansard/entries/375231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 375231,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375231/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Katika nchi ambazo zimebobea, tunaona kama nchi ya China kuna viwanda vidogo vidogo vingi ambavyo viko mashinani. Unapata ya kwamba hata unapotembea katika mitaa fulani unakuta pengine wanashughulika kutengeneza vijiko, mtaa mwingine wana kiwanda kidogo cha kutengeneza viberiti na haya yote ni kwa sababu wamejenga taifa lao na vijana wao kupitia taasisi hizi za kujenga ujuzi. Hivyo basi, kila sehemu imekuwa na viwanda na tunaona tunapata ajira nyingi katika nchi kama hizo."
}