GET /api/v0.1/hansard/entries/375235/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 375235,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375235/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wote ambao tunataka waweze kuendeleza nchi hii baada ya kuwa wamepata uwezo mwingi kupitia hizi tauluma. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, nimeona wakati mwingi sana nikitembea katika hizi taasisi zetu za vijijini kuna mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa yakipenda kujenga uwezo taasisi kama hizi lakini masikitiko ni kwamba wanafunzi huwa ni wachache kiasi cha kwamba kinawavunja nguvu. Tukiangalia, asilimia kubwa ya vijana wetu haijapata nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu vya Serikali. Wengi sana wanajiunga na taasisi ndogo ndogo ambazo ziko mashinani na hivi sasa kwa sababu tuko na mfumo wa ugatuzi pale mashinani, tutapata Wakenya wengi wenye ujuzi wa hali ya juu na kuweza kuleta ajira kwa wingi."
}