GET /api/v0.1/hansard/entries/375236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 375236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375236/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, napenda kujulisha Bunge hili ya kwamba vijana wetu wengi ambao hivi sasa wako nyumbani, si wengi hawana ujuzi. Wengi wamepata ujuzi mchache ambao wanataka kuuboresha na pengine kuwasaidia wenzao pia kuupata ujuzi huo. Iwapo kijana amesomea mambo ya kutengeneza magari basi anaweza kufungua kiwanda chake kidogo pale mtaani na pia kuweza kusomesha vijana wengine ili nao pia waweze kujikimu katika maisha yao."
}