GET /api/v0.1/hansard/entries/375237/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 375237,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375237/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, jambo kama hili tusiliangalie kwa uchache. Tunataka tuliangalie na tuliboreshe kwa ile azima yetu ama shabaha ambayo tunayo ya miaka 20 ama 30 ambayo ndio inayotusukuma sisi kama Wakenya kwa hivi sasa. Wabunge wenzangu, hivi sasa tunajua pia katika CDF tuna kiwango ambacho tunaweza kutumia kusomesha watoto wetu wanapojiunga na vyuo vyetu vya juu ama pia vyuo vingine. Pia tunataka pesa hizo tuzitumie kulipia karo wale ambao wanajiunga na taasisi hizi ndogo ndogo ambazo ziko mashinani na ambazo sisi wenyewe Wakenya tumezipigia debe. Sio tu kufikiria juu ya waliojiunga na vyuo vikuu. Tumetaka taasisi hizi ziwepo na pia tumelipa ushuru kuhakikisha ya kwamba zipo. Hivyo basi, tuwe tunaangalia pande zote mbili ndio tuone ya kwamba Wakenya wote walioweza kujiunga na vyuo vikuu na wale ambao pia pengine walifika darasa la nane ama kidato cha nne, wanapata ujuzi kupitia fedha hizi ambazo zinatoka katika mfuko mkuu wa Serikali yetu ya Jamhuri ya Kenya."
}