GET /api/v0.1/hansard/entries/375238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 375238,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/375238/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, hata nakumbuka Mheshimiwa Rais wetu akisema jinsi ambavyo ataweza kuboresha maisha ya vijana na akina mama. Alisema ya kwamba vijana wapate asilimia thelathini ya zabuni zote zitakazotolewa na serikali. Wakati wanapata zabuni kama kufanya ukarabati wa barabara ama kufanya ujenzi wa taasisi zetu zilizoko nchini kwetu Kenya, wanahitaji ujuzi na huo ujuzi utapatikana kwa taasisi kama hizi. Hivyo basi, tunavyoshirikiana katika njia kama hii na kutumia mikakati mwafaka kama hii, bila shaka tutaweza kuwa na Kenya tunayoitaka na Kenya ambayo itamfana kila Mkenya. Ataishi maisha ya kuheshimika na ataweza kujimudu katika maisha yake. Kwa njia hii, tutaweza kuondoa mambo ambayo yanafanywa sana na vijana, kama vile kushiriki madawa ya kulevya, kuingia katika pombe haramu na mambo ya ujambazi. Juzi tuu tuliona katika runinga ya kwamba watoto wadogo wa chini ya miaka 16 na 18 wameingia katika magengi ambayo yanafanya uhalifu wa hali ya juu. Sisi kama Wakenya tuko wapi na tunafanya nini juu ya jambo kama hili? Tunapochukua mkondo kama huu, bila shaka vijana kama hawa tutawatoa katika limbwi hili ambalo ni limbwi lakuwapoteza na kuwaangamiza katika mambo mabaya na maovu."
}