GET /api/v0.1/hansard/entries/377302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 377302,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/377302/?format=api",
"text_counter": 526,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Pili, kama tunavyojua, mara nyingi Serikali ni lazima ipate fedha za kuendeleza miradi yake. Miradi hii ni lazima iendelezwe kulingana na hali ya uchumi. Mara ya kwanza, tulikuwa na wasiwasi kuwa Hoja hii ikiletwa na ikiendelea vile ilivyokuwa, ingeuhujumu uchumi wetu na ingewatatiza wanyonge na watu wa kima cha chini kwa hali ya chakula, malazi, shule na kadhalika. Lakini Hoja hii iliporudishwa Bungeni, imefanyiwa marekebisho kadha wa kadha na inaambatana na mahitaji ya wananchi. Kama inaambatana na mahitaji ya wananchi, ni muhimu tuiunge mkono ili Serikali ipate fedha za kutosha za kuendeleza miradi yake. Tatu, kupitia Hoja hii, ambayo imekuja wakati unaofaa, Serikali ina nia ya kuona kuwa yale majukumu ambayo ilikuwa imejipatia ama majukumu ambayo ilikuwa inatarajia kutimiza, itatimiza. Kwa hivyo, ninachukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii kikamilifu bila tashwishi yoyote. Ninaomba Wabunge wenzangu waiunge mkono."
}