GET /api/v0.1/hansard/entries/377714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 377714,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/377714/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii. Ninakumbuka kwamba wakati wa Kibaki aliweka pesa nyingi sana katika Banki ya Equity ili zisaidie vijana. Si vijana wote walifaidika kutokana na zile pesa. Kwa mfano, katika jamii ya Wameru, wakati wa vita baada ya kura za mwaka wa 2007/2008, mabasi yalibeba vijana kutoka Eldoret wakamwagwa huko Meru katika mji wa Kolomone. Waliletwa na basi zaidi ya tano. Asubuhi yake waliamkia kwenda kwa Banki ya Equity pale Makutano na tawi lingine karibu na Msikiti Mjini Meru. Kila mmoja wa wale vijana alipata Kshs50,000, ambazo walitumia kununua bidhaa za uchuuzi. Naibu Spika wa Muda, vijana wetu ambao walikuwa wanafanya kazi ya uchuuzi kule Meru, wote waliondolewa! Wengine ambao walikuwa wanafanya kazi kama vinyozi pia waliondolewa wote. Kabila moja pekee ndilo lilifaidika kutokana na pesa za vijana. Kama pesa za vijana zinakuja, ni lazima ziwafaidi vijana kutoka Kenya nzima lakini si kabila moja. Ninaunga mkono."
}