GET /api/v0.1/hansard/entries/377880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 377880,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/377880/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa nadhani sitapata muda wa kuongea kwa sababu nimengoja sana. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kwa kweli, sheria ilikumbuka wanyama pori ikasahau binadamu. Wanyama pori wamekuwa kero kubwa sana katika eneo la uwakilishi Bungeni la Mwatate na vile vile Jimbo la Kaunti ya Taita Taveta. Wiki mbili zilizopita, simba walikula mbuzi zaidi ya kumi na ng’ombe zaidi ya tano, mali ya mkaaji wa eneo la uwakilishi Bungeni la Mwatate. Ni nadra sana mvua kunyesha katika maeneo hayo. Wakaaji wa hayo maeneo wanawategemea tu hao wanyama wa kufuga. Msimu huu uliopita, mvua ilinyesha vizuri na watu wakapanda mimea yao sawa sawa. Lakini baada ya muda mfupi, ndovu waliharibu hiyo mimea yote. Hata sijui tutafanya nini. Maanake nikiangalia huku, mshahara umempunguzwa kidogo na Serem na hatuna hata kiwanda kimoja kule. Kwa jumla, wanyama wa pori wameumiza watu wengi. Mzee mmoja aliumizwa na ndovu. Ako na watoto shuleni lakini hawezi kufanya shughuli yoyote kwa sababu amelemaa. Akienda kutafuta fidia kutoka KWS, hakuna kitu ambacho kinapatikana. Hoja hii ni nzuri sana na ningeomba tuangalia Mswada ambao utaletwa hapa Bungeni ili tuweze kutatua shida ya wanyama wa pori na binadamu. Tunafaa kuangalia vile binadamu wanavyoweza kufaidika wakati wameumizwa au mimea yao imeharibiwa na wanyama wa pori. Hii inafaa kuwa sambamba kama vile binadamu akiumiza wanyama. Hawa wanyama wameishi na binadamu kwa muda mrefu na sio kuwa wana akili kuliko binadamu. Ninavyoongea sasa, wakaazi wa eneo Bunge langu wanauliza watafanya nini kama watu wa KWS hawasikii na watatumia njia gani kuwamaliza wanyama. Kama unavyofahamu, njia ni nyingi. Ingawaje tunafahamu kuwa wanyama pori wana faida kwa upande wa utalii, hawa watu ambao wanakaa na wanyama pori katika eneo hilo, hawafaidiki kwa njia yoyote kutokana na utalii. Kwa jumla, kuna matatizo mengi kati ya wanyama pori na binadamu."
}