GET /api/v0.1/hansard/entries/377883/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 377883,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/377883/?format=api",
    "text_counter": 312,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Naunga mkono Hoja hii ya mhe. Njuki kwa sababu kama vile wanyama pori wanavyowasumbua kule Mlima Kenya, kule Tsavo hi hivyo hivyo. Vile vile, naunga mkono mhe. Nyikal ambaye ameongea muda mfupi uliopita. Ni lazima tuangalia fidia kwa watu wanapoumizwa na wanyama wa pori. Vile vile, tuangalie fidia watu wanapoadhiriwa. Wasipatiwe pesa kidogo. Mhe. Njuki ametaja Kshs1 milioni lakini nadhani kuwa katika Mswada utakapoletwa Bungeni, tutaangalia vizuri na tuchangie zaidi. Nikisikia watu wakiongea juu ya jambo hili, ninawashwa. Nahisi kama fimbo inanichapa na kuna maumivu kwa sababu wanyama wa pori wametusumbua sana. Nitangojea Mswada uletwe hapa Bungeni ili nichangie zaidi. Naunga mkono Hoja hii."
}