GET /api/v0.1/hansard/entries/380242/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 380242,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380242/?format=api",
    "text_counter": 28,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "sehemu kubwa ni ya wafugaji. Lakini inadhihirika na kukubalika kwamba wafugaji wanatoka katika sehemu za kaskazini mwa Kenya tu, ambayo sio desturi nzuri na sio ukweli kabisa. Wanajaribu kuwadunisha wafugaji kuwa watu wachache sana nchini ili kusudi wasipate mapato na kupewa haki zao kutoka kwa uchumi wa Serikali. Nafikiri kwamba katika Kenya nzima, zaidi ya nusu ya watu ni wafugaji. Tukisema kuwa ufugaji sio ng’ombe na ngamia tu; kuna mbuzi, kondoo, kuku, samaki na kadhalika. Lakini huu ni uchumi ambao kwa kweli, haujatiliwa maanani, kama vile Sen. Kajwang alivyosema. Alitoa mfano wa hivi majuzi, ng’ombe walipofariki huko kaskazini mashariki mwa Kenya kichinjioni. Hata hivyo, mizoga hii iliangaliwa tu na wakasahau kwamba katika hiyo mizoga ya ng’ombe kulikuwa na ngozi yenye thamani kubwa. Ngozi hii ingechunwa na kuleta uchumi mkubwa nchini, lakini mali hii iliwachwa ikaangamia na kuzikwa. Hiyo ni aibu! Viwanda vya ngozi tangu wakati wa Uhuru vilikuwepo---"
}