GET /api/v0.1/hansard/entries/380263/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 380263,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380263/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Lakini sasa, hayo ninayosema ni ya kweli; kama huyataki, ni sawa, kwa sababu pilipili usiyoila yakuwashiani? Twataka hivi viwanda vijengwe kila mahali, haswa tuangalie uchumi utokanao kwa ngozi. Sio vizuri – ama niseme sio halali – sisi tukiwa wafugaji walio na mifugo wengi, kuona raslimali yetu ikipotea, halafu twaagiza viatu kwa bei ghali kutoka nchi za nje. Huo ni ujinga, ubaradhuli, ukosefu wa hekima na kadhalika. Lazima tugutuke na tujue kwamba kuna sehemu nyingi ambazo tunaweza kutoa mifugo mingi yenye afya nzuri inayoweza kuchinjwa ikiwa bado hai ili Waislamu pia wafurahi. Katika sehemu za Nyanza, kama Lambwe Valley, tuna taabu ya Mb’ung’o – wadudu wanaouma ng’ombe na kuwapa maradhi ya usingizi. Serikali imeweka hili jambo kando; haliangaliwi kwa maanani na twapoteza mifugo mingi sana. Hizo ni sehemu ambazo ukiondoa tu kile kipande ambacho kina sehemu ya wanyama, sehemu nyingine hazina watu; sehemu ambazo zingetumika kufuga mifugo. Lakini hata hivyo, sisi tunajulikana kweli kama watu ambao wanaopoteza raslimali kiholela holela. Kwa mfano, Ziwa Victoria limejaa maji tele yanayotumika huko Misri na kadhalika, wakitumia mkataba uliowekwa wakati huo wa ukoloni. Ethiopia wamegutuka na wameanza kutumia raslimali ya maji yao ilhali sisi bado twasema “bado twafuata mikataba hiyo!” Kwa nini maji hayo yasitekwe, yavutwe kwenye mifereji mpaka sehemu za juu halafu yawachwe yateremke yenyewe bila ya kutumia mashini? Maji haya yakiwekwa katika maeneo makubwa ya muinuko ya Bonde la Ufa katika sehemu za Kisii, yatatiririka bila mashini katika Nyanza nzima kunyunyizia mazao na manyasi yalioko. Tutapata mazao ya hali ya juu; na sio mazao ya kulima ya nafaka tu, bali pia mazao ya Wanyama wetu; ng’ombe, kondoo, mbuzi na hata ngamia wafugwe huko na watakua. Hili jambo lililoletwa katika Mswada huu – ingawa simuoni hapa mwenye Mswada – ni jambo zuri. Huu ni mpango ambao ukitekelezwa na ukifuatiliwa kwa dhati, waweza kuinua uchumi wa Kenya tukawa na raslimali ya kuweza kujenga maeneo yetu ya Majimbo yaliyoanzishwa Kenya hii. Ni jambo la kuzingatiwa kwamba wafugaji wapewe viwanda vya kila aina; sio viwanda vya ngozi tu, bali pia viwanda vya kuchinja mifugo na kufadhili nyama. Hatutaki wawe wanachinja tu na kuanza kusomba mizoga kuleta Nairobi ili iuzwe; twataka nyama hiyo iwekwe ndani ya mikebe---"
}