GET /api/v0.1/hansard/entries/380348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 380348,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380348/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Namshukuru pia Sen. Lesuuda kwa kunipa fursa hii. Naunga Hoja hii mkono na ningependa kusema kwamba jambo la ufugaji linahitaji liangaliwe sana. Ufugaji ulikuwepo tangu jadi lakini wafugaji wamesahaulika kimaisha na Serikali yetu. Serikali haikutia maanani mambo ya ufugaji kwa sababu hawakupata usawa na ndugu zetu wengine wakulima. Ufugaji ni njia pekee ambayo wafugaji wanaweza kupata mapato. Mimi kama mfugaji ni mchungaji wa kuhamahama. Hiyo sehemu ambayo tunaishi inahitaji ufugaji kuimarishwa kwa usawa kama wengine. Wakati mfupi uliopita nilisikia Serikali ikisema kwamba sehemu ambayo ilikuwa imetengwa ya ADC Galana itafanyiwa ukulima lakini ufugaji unazorota na unahitaji uangalifu zaidi na pia kuinuliwa. Kwa hivyo tunasema kwamba tunataka ufugaji uwe sawa na sehemu zingine za maisha. Sisi wafugaji tunategemea---"
}