GET /api/v0.1/hansard/entries/380431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 380431,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380431/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chiaba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 3,
"legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
"slug": "abu-chiaba"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niungane pamoja na wenzangu kuzungumza juu ya Hoja ilioko mbele yetu. Vile vile namushukuru Sen. Kagwe kwa kuleta Hoja hii mapema, kwa sababu ni muhimu sana. Ukiangalia vile tunafanya kazi kama Bunge, Kamati zote zilizoko zinaweza kukaa na kuchunguza Bajeti inayoletwa na Serikali. Vile vile ni muhimu kuwafundisha au kuiambia idara inayohusika kuzifundisha bunge za Kaunti kutumia komputa. Pia ningependekeza kuwa badala ya kutumia Kiingereza watumie lugha ya taifa ili wakija kwa Bunge au Seneti, waweze kufanya mijadala kwa lugha ya taifa. Hiyo ndio njia moja ya kujikomboa kutoka kwa minyororo ya wale waliopita. Sisemi ya kwamba lugha ya Kiingereza ni mbaya, lakini kila mtu hujivunia lugha yake mwenyewe. Ni muhimu kuzipatia bunge za kaunti komputa na kufundishwa kikamilifu, ili waweze pia kuchunguza zile bajeti zinazofanywa na magavana au kamati kuu za magavana, ili watu waone kuwa walichagua bunge za kaunti ambazo zinaangalia maslahi yao. Vile vile ni muhimu kwa wanahabari walio katika bunge za kaunti na pia wale walio hapa na pia katika Bunge la Kitaifa wawaelimishe watu wasiokuwa katika bunge za kaunti kuhusu kitu gani kinachofanyika katika bunge hizo na masilahi yao yanachukuliwa namna gani. Vile vile, ni muhimu Spika wote wawili wa Seneti na wa Bunge la Kitaifa kufanya kongamano maalumu kuwafundisha maspika wote wa bunge 47 za kaunti ili kuwaelezea njia bora za kuendesha kazi ya bunge hizo. Kwa hayo machache, Bw. Spika wa Muda, naomba kuunga mkono. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}