GET /api/v0.1/hansard/entries/380448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 380448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380448/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kama vile wenzangu walioongea mbele yangu walivyofanya, mimi pia naunga mkono Hoja hii. Bw. Spika wa Muda, nakubaliana na Seneta wa Laikipia, Bw. G.G Kariuki, kwamba vile tunazihimiza serikali za kaunti zifadhili au zilete hali hii ya maendeleo kwa kuwapa uwezo wabunge katika bunge za Kaunti kuweza kutekeleza majukumu yao, huu kwa ukweli ni ushauri. Sisi tunawahimiza kuwa ni lazima waweke misingi na mikakati kwa vile hakuna namna. Kenya imepiga hatua katika mawasiliano na pale ambapo hatujapiga hatua ni lazima tupige hatua katika mawasiliano kama hayo. Kwa mfano, katika Chumba hiki ambamo tunakutana kama Seneti, ni lazima tuweke vifaa vya kisasa ambavyo vitaweza kuturahisishia sisi kuendeleza ratiba ya Seneti, mabunge ya kaunti na Bunge la Taifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}