GET /api/v0.1/hansard/entries/380452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 380452,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/380452/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wakati kuna haja ya kuibadilisha, ofisi ya Katibu wa Seneti anaweza kuweka mabadiliko hayo na unayapata papo hapo. Natumahi kuwa lile Chumba la Seneti ambalo linajengwa limewekwa vifaa kama hivyo ili kuhakisha kuwa tunaweza kupata teknolojia na kuitumia. Hii inafaa kuwa ratiba katika Bunge letu la taifa na pia mabunge yetu ya kaunti. Kwa hivyo hakuna haja ya kubebana na makaratasi kila wakati. Nikija hapa nataka kubonyeza kitu na kujua kuwa hii ndio ratiba, hii ndio Miswada itakayokuja saa nane na hapa ndipo tumefikia na kukomea. Hata nimewaona wenzetu kutoka kwa ofisi ya Katibu wa Seneti wamefurahi kwa sababu hawataki mambo ya photocopy kila wakati. Tunafaa kuweka hatua kama hizo. Bw. Spika wa Muda, pili, katika ushauri huu sisi pia kama Seneti ni lazima tutoe mwongozo, kama vile Bw. Obure alisema. Tunafaa kuwa na master-plan ambayo itatoa mwongozo kuwa lazima mabunge yote ya kaunti yawe na viwango fulani katika majengo yao na ofisi zao, ili yaweze kuendeleza ratiba zao. Kama kweli tunaamini ugatuzi, ni lazima tuweke kiwango cha juu cha---"
}