GET /api/v0.1/hansard/entries/381063/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 381063,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381063/?format=api",
    "text_counter": 46,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Nyakeriga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13112,
        "legal_name": "Linet Kemunto Nyakeriga",
        "slug": "linet-kemunto-nyakeriga"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuunga Hoja hii mkono. Kwanza kabisa, namshukuru Sen. Elachi kwa kuleta Hoja hii hapa. Pili, ningependa kuchangia kwa kusema kwamba kwa kweli tumewakumbuka vijana, haswa walemavu. Kwa upande wa walemavu, unapata ya kwamba sisi hatuna shule ambayo inawafunza vijana. Kwa hivyo, yatakikana vijana wawe waangalifu na wafanye zile kazi wanazopewa. Ningependa pia kuomba kuwa Serikali inapoajiri, iajiri vijana na ikumbuke walemavu kwa sababu vijana walemavu wako na nafasi chache zaidi. Tukiangalia haswa wakati askari wanapoajiriwa, vijana walemavu hawawezi kufanya kazi ya uaskari. Kwa hivyo, tunafaa kuwaangalia kwa upande huo pia. Nashukuru Serikali kwa kutukumbuka sisi vijana ili nasi pia tuweze kupata kazi. Kwa hayo machache, naomba kuunga Hoja hii mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}