GET /api/v0.1/hansard/entries/381072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 381072,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381072/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Spika, nashukuru kwa nafasi hii ili niweze kuongea juu ya Hoja hii. Sen. Elachi, ametukumbusha kwamba Kipengele cha 43 cha Katiba yetu kinawapa nafasi vijana wapewe haki yao kiuchumi katika hali ya maisha. Pia Sura ya 13 ya Sheria za Kenya, Kipengele cha Sheria 208, kinampa Waziri anayehusika uwezo wa kujenga vituo hivi vya jeshi la vijana wa Kenya popote anapotaka. Yeye anaomba kwamba jeshi hili litawanywe na kuwekwa kwa kila jimbo nchini. Sio kwamba tunahitaji sheria mpya, kwa sababu sheria ipo na sio kwamba tunahitaji mamlaka mapya kwa sababu yapo, bali ni kumpa wasia Waziri anayehusika kwamba yuko na uwezo na ataanza kusambaza haki ya huduma hii kwa vijana wetu. Jeshi la vijana wa Kenya limeandaliwa hapa nchini kwa miaka mingi, likatumika vile na vile lakini nakumbuka kwenye mwaka wa 2004, jeshi hili lilitumika kwa kukusanya vijana ambao wanaranda randa mjini Nairobi na miji mingine. Walipelekwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}