GET /api/v0.1/hansard/entries/381074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381074,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381074/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwa mafunzo kadhaa wa kadhaa. Sisi hatujafahamu ni fundisho gani tulilolipata kwa jambo hili. Hawa vijana walipotoka, walienda wapi, waliajiriwa wapi, ni wangapi walifaulu kwa maisha yao na ni wangapi walirudi barabarani kuomba omba. Tunahitaji kuambiwa mpango huo ulifikia wapi. Lakini kuna ishara kwamba mpango huo uliishia hapo. Baada ya vijana kujua kwamba wanachukuliwa kutoka barabarani, basi wengi walijitupa barabarani kusudi wakusanywe na wapelekwe kwa jeshi la vijana wa taifa. Bw. Spika, sio lazima tuangaze mawazo yetu kwamba ni wale ambao wamemaliza Kidato cha Nne tu bali kuna wale vijana ambao pia wana uwezo na wamemaliza Darasa la Nane lakini kwa sababu ya hili na lile hawakuweza kupata elimu nyingine. Kwa hivyo, ningesema kwamba sio tu kuandaa na kuanzisha vituo hivi lakini vianzishwe vituo vya madaraja tofauti tofauti. Hivyo ni vituo ambavyo vinaweza kuelimisha yule kijana ambaye amemaliza darasa la kumi na mbili au Kidato cha Nne na vingine ambavyo vinaweza kuanzisha huduma za elimu kwa vijana ambao wana masomo nadhifu hata kama ni wa Darasa la Saba au wale ambao hawakupata nafasi ya kwenda shuleni kwa sababu sio kila mahali ambapo watu wote wamepata nafasi ya kuelimika. Hata hivyo ingekuwa vizuri kwamba jeshi hili lingejiandaa kutoa nafasi za elimu na mafunzo tofauti tofauti kwa kila kituo. Hakuna haja kwamba kila kituo kitoe nafasi ya kufundisha mambo yote kwa kituo kimoja. Kwa mfano, Migori ichukue mafunzo ya uandishi, Kakamega ichukue mafunzo ya upishi, Pwani ichukue mafunzo ya uvuvi na kadhalika. Sikusema hivyo kwa sababu nataka hivyo lakini nimetoa mfano tu. Nisije nikaeleweka vibaya. Hii ni kusudi kwamba watu wa eneo fulani wanaweza kutoka jimbo fulani na kwenda jimbo lingine ili mradi wapate elimu fulani na hapo basi kuna nafasi ya vijana kuchanganyika na kuwa na mawazo ya kizalendo badala ya kuwa na kituo kimoja ambacho masomo yote yanapatika. Haya masomo yawe ambayo yanaweza kuwapa vijana uwezo na uadilifu kuwa wataalamu kwa nafasi hizo ambazo wamepewa kusomea na wasirudi nyumbani tena kusumbua watu kwamba hamna kazi. Inafaa wawe wamepewa masomo ambayo yanaweza kuwapa uwezo wa kujiajiri. Haya masomo ni kama uhunzi, umekanika na kadhalika. Tukifanya hivyo kwa mpango bora, basi tutafaulu. Sio lazima kwamba jambo hili likienezwa kwa majimbo kwamba ni lazima wanafunzi hao waishi kituoni. Kwa sababu jambo hili limeenda mashinani, basi wanafunzi wengine ambao hawana uwezo wengine wanaweza kutoka nyumbani na waje kusoma. Wakitoka nyumbani gharama itakuwa chini na nafuu ili mradi huu usambazwe kila mahali. Hili ni jambo nzuri na ni la hekima. Hili ni wazo nzuri ambalo Sen. Elachi ameleta, kwa hivyo yafaa litiliwe maanani na kutekelezwa ili tufaulu. Asante. Naunga mkono."
}