GET /api/v0.1/hansard/entries/381078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381078,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381078/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Bw. Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili niweze kuunga mkono Hoja hii. Hoja hii ni ya muhimu sana. Hoja hii inaangazia matatizo ambayo yanatukumba kwa njia tofauti tofauti kutoka kaunti zetu. Maswala ya vijana ni ya kusikitisha sana. Asilimia 70 ya vijana haswa kule ninakotoka ni watu wa kurandaranda na ni watu ambao hawana kazi. Hawa ni watu ambao wamebaki nyuma kimaisha. Kwa hivyo, ni lazima Serikali iangazie swala hili na iwe na njia mwafaka inayowezesha kuleta maisha yao sawa na wengine. Bw. Spika, Kipengele cha 27 cha Katiba kinasema kwamba kila mmoja ana haki sawa na mwingine. Kwa hivyo, yule kijana ambaye hajasoma yuko na haki sawa na mwingine ambaye amesoma. Kwa hivyo, tunasema kwamba Hoja hii ni ya muhimu na yafaa Serikali itilie maanani ili tuwe na mahali pa kuhifadhi na kuwafundisha vijana hawa. Ujana ni kiungo muhimu katika maisha ya mwanadamu. Ujana ni umri ambao kila mtu anapitia na kila mmoja anajua shida ya ujana. Vijana hawa hutumika vibaya, vijana huwa shiftas na hutumiwa kuchukua ng’ombe wa wenyewe na kuuwa watu. Vijana pia hutumiwa na wanasiasa na kadhalika. Kwa hivyo, tusipowatumia vijana vizuri, basi tatizo halitatoka kati yetu. Kwa hivyo, ningeomba Serikali ichukulie Hoja hii kwa maanani. Kila kaunti yafaa iwe na mahali pa vijana. Yafaa tuwe na mahali pa kufundisha ama kurekebisha vijana ili kila kijana akitoka huko awe anaweza kupata elimu ambayo inaweza kumnufaisha usoni. Kwa hivyo, ninaunga Hoja hii na kusema kwamba ninashukuru mwenye kuileta. Aliweza kukumbuka kwamba vijana ni muhimu na ni hatari. Tusiseme kwamba kijana ni yule wa Darasa la Nane bali kijana yeyote wa Kenya. Kuna wengine huwa wanaitwa chokora na ndio wanaleta matatizo. Wale ambao wanaleta matatizo ni wale ambao wamekosa nafasi huko mbele; wale ambao wazazi wao walikosa kuwapeleka shuleni. Kwa hivyo, wale ambao wamepata fursa ya kupata rasli mali Kenya hii ni wale ambao wazazi wao waliweza kusoma na kufanya biashara. Jana katika magazeti, kuna picha za vijana; zilikuwa zimewekwa kwa gazeti kwamba wamepotea na wanatafuta wazazi wao. Vijana kama hao hawawezi kujua wazazi wao. Kwa hivyo, kuna matatizo huko mbele kwa sababu tusipowaangalia vijana hawa, wazungu wanasema, spare the rod and spoil the child . Mtoto asipolelewa vizuri hatakuwa mzuri. Juzi nilisikia kwamba Al Shabaab wananyemelea Kenya na kuchukua vijana. Kwa hivyo, tutakuja kupata Amerika imewachukua vijana wetu. Pia, vijana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}