GET /api/v0.1/hansard/entries/381080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381080/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "watakapokufa nchini Somalia, vijana wetu watachukuliwa kutoka hapa ilI waende wakatumiwe vibaya. Tunataka kuwa na mafundisho ya vijana. Sehemu hizo za mafundisho hazifai kutumika kuwafundisha askari. Hapana! Askari hufundishwa kuua. Mtu ambaye ni askari hafai kuwa mwanasiasa. Askari ni mlinzi. Tunataka vijana ambao wamefundishwa kazi mbali mbali kama vile kazi ya kujenga nyumba, kupiga randa, kupiga tarumbeta na huduma zingine ambazo tunahitaji. Vijana wanapohitimu masomo hayo hawafai kuwachiliwa. Wanafaa kuonyeshwa kazi ambazo wanayoweza kufanya. Tunataka vijana wajue kupiga randa kwa sababu kazi hiyo huwa haihitaji masomo mengi. Madereva wa malori na magari ambayo huenda safari ndefu kama vile Uganda, Burundi na Tanzania hawajasoma lakini wao huenda na kufika. Utaona Msomali akifanya biashara bila kuwa na masomo. Watu hawa hufanya biashara na kuwa na maisha mazuri hata kuliko Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o, na watu wengine ambao wamesoma."
}