GET /api/v0.1/hansard/entries/381136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381136/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, leo tumeamua tuendelee kwa lugha ya Kiswahili. Mimi ningependa kuzungumzia mambo mawili ambayo ni muhimu sana. Sisi kama taifa la Kenya, tumepewa utajiri mkubwa sana katika upande wa mazingira. Sijaenda katika taifa lolote ambapo nimeona utajiri kama tulionayo. Tuko na mabonde, bahari, mito, nyika na kadhalika. Wageni wengi wakija hapa husema tuna kila kitu ambacho kinaweza kukuza uchumi wetu. Lakini kwa sababu ya ukosefu wa mipangilio maalum ya Serikali na utovu wa nidhamu wa raia wetu kwa jumla, utajiri huu hautusaidii. Sisi ni maadui wakubwa wa mazingira yetu. Tumeuharibu utajiri wetu tuliopewa na Mungu. Hili ni jambo la kisiasa. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu ni lazima tulinde na tutunze mazingira yetu. Huu ni utajiri ambao tumepewa na Mungu. Kama vile Kiongozi wa Wengi alivyosema, ni utajiri ambao tunafaa kuudhibiti kwa niaba ya kizazi hiki na vizazi vijavyo. Vizazi vitakavyokuja ni lazima viishi katika mazingira ambayo yanaweza kujidumu. Mimi ninamshuruku yule aliyeleta Hoja hii. Sisi kama wanasiasa hatuna ujasiri wa kufanya mambo mazuri kwa sababu tunaogopa kuwa siku ya uchaguzi itakapokuja, watu ambao tuliwaambia waondoke katika fuo za mito watapiga kura pande nyingine. Wanasiasa ambao wamekaa hapa kupitisha Hoja hii ndio watakaopigwa watakapotaka kutekeleza mambo haya. Ni lazima Wakenya wafahamishwe mambo haya. Tunajua watu wetu wanatafuta riziki za kimaisha. Lakini hali zao haziwezi kuyahatarisha mazingira yetu na maisha kwa jumla. Mtu ambaye anajua anafanya kitu ambacho kinaweza kuleta madhara ya kudumu kama vile mchafuko katika mito na mazingira yetu ni lazima tutumie njia za kisheria kumtia kikomo. Tunataka Wakenya kwa jumla, wale walio sasa na wale watakaokuja baada yetu warithi mazingira ambayo yamedumishwa na sisi. Tunafaa kuwa na mazingira ambayo yanaleta afueni katika maisha yetu sisi sote. Jambo la mwisho katika kuchangia Hoja hii ni kwamba wanasiasa wanafaa kushirikiana na Serikali inapofanya kazi ambayo ni ya manufaa kwetu sisi sote. Tukisema tunataka kwenda Tana River kuhifadhi mazingira, Sen. Bule hafai kukataa ama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}