GET /api/v0.1/hansard/entries/381138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381138,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381138/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwa na shida yoyote. Hafai kulifanya hili kuwa jambo la kisiasa. Lazima watu waelimishwe. Wanasiasa wanafaa kuwa katika mstari wa mbele katika kuhakikisha tunawaelimisha watu wetu ili wayaelewe majukumu yao. Wanafaa kuelewa kwamba kuna majukumu na haki zao pia lakini kuna haki za kijamii na taifa la Kenya kwa jumla. Kwa hivyo, haki zako na maisha yetu sisi sote ni lazima ziangaliwe. Hata hivyo, kuhifadhi mazingira yetu ni jambo ambalo tunafaa kulizingatia kama Wakenya na kama wanasiasa. Tuliona Serikali zilizopita zikipora mazingira yetu. Walijigawia ardhi za umma na kupora mali za kiasili. Tulipowaonya dhidi ya kufanya hivyo, siasa zikazuka na kutawala akili zetu. Jamii fulani ilianza kusema inadhulumiwa na kuonewa. Ni lazima tuseme ukweli katika maswala ya kisiasa, mazingira na maisha yetu. Nataka kumhakikishia Sen. Kittony kwamba tuko katika taasisi moja na tutahakikisha tumetekeleza Hoja hii. Mtu yeyote akisimama kati yetu tutamwambia anatukosea ili tusonge mbele na kuhifadhi mazingira yetu. Hoja hii haitaki Mkenya atolewe katika mazingira yake. Hoja inaomba tuwaelimishe Wakenya wote juu ya faida za kuifadhi mazingira yetu. Hatufai kuleta mchafuko katika mazingira yetu na katika maji yetu. Maji hutupa uhai. Wakenya wakielimishwa na kufahamu majukumu yao watajua miradi ambayo wanafaa kutekeleza. Wale ambao wataendelea kupora mazingira yetu hatutakuwa na namna ila kuwachukulia hatua za kisheria. Sheria hii inafaa kuzingatia vile itahifadhi maswala ya kisiasa. Mara nyingi sisi wanasiasa huwa adui wa zile sheria tunazopitisha katika Bunge letu. Leo tumeonyesha ya kwamba tunajua kuzungumza Lugha ya Kiswahili. Hii ndio mara yangu ya kwanza kuzungumza Lugha ya Kiswahili katika Seneti hii. Mhe. Obure alisema Lugha ya Kiingereza ilikuja na mashua. Kama mashua ilitia nanga katika ufuo wa Pwani, basi ni sisi tuliyopokea Lugha ya Kiingereza kwa mikono miwili. Sisi ni Waswahili."
}