GET /api/v0.1/hansard/entries/381426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 381426,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381426/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gertrude",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Elachi kwa kuleta Hoja huu. Leo nina hakika kwamba kama kuna vijana wanaoangalia runinga, wataona kwamba kwa mara ya kwanza, Seneti imeweza kuongea masuala yanayohusiana na vijana. Ninampongeza Sen. Elachi. Hoja hii inalenga watoto maskini kule mashinani na ikiwa itapitishwa, ninaamini kwamba suala la MRC litatatuliwa. Mara nyingi kumekuwa na recruitment ya wanajeshi na vijana wetu wamekosa kuchukuliwa kwa sababu kila kitu kilikuwa kikifanyika huku juu na sio mashinani. Kama kutaanzishwa mambo kama haya kwenye kaunti, basi huenda vijana wetu watajiona wamekumbukwa na watapata kazi ya kufanya. Tukiangalia kwetu pwani, vijana wengi wakifika sekondari wanashindwa kuendelea na masomo kwa sababu hatuna ajira yoyote ya kuweza kusomesha watoto wetu. Kwa mfano, mimi sikuwa na baba, mama yangu hakuwa na title deed na sikuweza kuendelea kusoma. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}