GET /api/v0.1/hansard/entries/381428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381428,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381428/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gertrude",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Asante sana. Mama yangu hakuwa na cheti cha kumiliki ardhi ambacho pengine angepeana kwa benki na akapewa mkopo. Pengine ningesoma zaidi na nikawa kama wenzangu. Kwa hivyo, huu ni mjadala mzuri ambao kama Maseneta wengine wangekuwa hapa, leo kungekuwa na changamoto nzuri sana ya kuweza kufafanua Hoja hii zaidi. Ningetaka kusema kwamba Hoja hii itakapozaa Mswada na kuwa sheria ili NYS iweze kupelekwa kwenye kaunti, sheria zisiwe kama zile za jeshi letu wakati wanapofanya recruitment . Ningependa wazingatie umri. Mara nyingi nyingi huwa wameweka kiwango cha umri na watoto wa kwetu wa Kimijikenda wanasoma kuchelewa. Wanapofika sekondari hao huwa hata miaka 27 na wakati mwingine huwa wameoa. Ningesisitiza kwamba kusiwe na ubaguzi wa kikabila katika kufanya recruitment kwa sababu kuna Wakikuyu na Wajaluo waliozaliwa kule pwani. Inafaa masuala haya yatiliwe maanani wakati wa recruitment ya NYS. Hawa ni watu ambao kama hawachukuliwi, wataenda wapi? Wakati mwingine vijana hutakikana wasiwe na kovu, ilhali wakati wanapocheza mpira huwa wanaumia. Kijana akipatikana na kovu huwa hawachukuliwi kwenye NYS kwa sababu ya kovu. Ni lazima Serikali itilie maanani kwa sababu vijana wetu wote wanaumia wanapocheza na ni lazima watakuwa na kovu. Ninaunga mkono. Asante."
}