GET /api/v0.1/hansard/entries/381495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381495/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii. Pia mimi ningependa kujumuika na Maseneta wenzangu na Wakenya wengine kuomboleza vifo vya wanafunzi vilivyotokea kule Kisii. Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na wana akili sana. Kama tunavyojua, ukisomesha mwanafunzi umesomesha taifa nzima. Maisha yao yamekatizwa kwa wakati ambao haujafika. Mimi, familia yangu na watu wote wa Kilifi County ningependa kuwapatia pole sana wazazi wa watoto hawa, familia na jamii zote za watu wa Kisii haswa nikizingatia sana Gavana ambaye ni rafiki yangu, Gavana Ongwae. Ninajua ana wakati mgumu sana wakati huu. Pia ningependa kumwambia kwamba aweke juhudi zake za kuweza kusaidia familia zilizokumbwa na vifo hivi. Pia vile vile ndugu yangu Mbunge wa eneo hilo, Mhe. Jimmy Angwenyi, ili aweze kupata nguvu ya kusaidia familia. Sitamsahau pia Seneta wetu ambaye tuko na yeye hapa; Sen. Obure na dada yetu, Sen. Ongera. Najua kwamba ni watu ambao wanaangaliwa kule nyumbani. Kwa hivyo, mimi ningependa kuwatia moyo na kujua kwamba Wakenya wote wanaomboleza. Pia vile vile tumeona katika hizo harakati, Serikali imeungana pamoja na watu wote wa Kisii kuona ya kwamba kumekuwa na usaidizi wa kutosha kupeleka watoto hao katika shule. Tumesikia na tumeona kwa televisheni kwamba watoto ambao wameumia zaidi wameletwa hospitalini. Tunawaombea Mwenyezi Mungu ili wale ambao wako hai waweze kuepuka hasara hiyo. Wale wazazi ambao waliathirika na vifo hivyo tunawapa pole sana na tunaomba ya kwamba Mwenyezi Mungu aweze kuweka roho zao pahali pema peponi. Bi Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba ni jambo la kusikitisha kuona kwamba mara nyingi hata sisi wenyewe tukiwa katika hali ya usafiri usiku tunashindana na mabasi ambayo yamejaa wanafunzi. Hii ni usiku wa maanane. Ile basi ya wanafunzi huwa inaendeshwa kwa hali ambayo,sio ya uangalifu. Tunataka, ikiwa itawezekana kuwe na hatua ambayo itazuia mabasi ambayo yamebeba watoto wa shule kutembea baada ya saa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}