GET /api/v0.1/hansard/entries/381499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381499,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381499/?format=api",
"text_counter": 330,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Elachi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13115,
"legal_name": "Beatrice Elachi",
"slug": "beatrice-elachi"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kujiunga na wenzangu kutuma rambi rambi zangu kwa niaba pia ya akina mama, ndugu zangu kule Kisii na pia kwa niaba ya Serikali. Ningependa kushukuru Serikali na ninajua kwamba itaendelea kusaidia kama ilivyofanya jana. Jambo la muhimu ni kujiuliza ni kwa nini wakati mwingi sisi huwa tunasahau kwa haraka maswala kama haya yanapofanyika. Ukikumbuka watoto wa Loreto ambao walikuwa wanatoka kule Meru na wakapata ajali, ilibidi wengine wao wafanye mtihani bila mikono na mpaka wa leo ni walemavu. Tunajua kwamba watoto hawa watakuwa walemavu na tunajua kwamba hatuna vile tutaendelea kuwasaidia wanapougua."
}