GET /api/v0.1/hansard/entries/381519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381519/?format=api",
"text_counter": 16,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "RESTORATION OF KENYA’S COMPETITIVENESS THROUGH EXPANSION AND MODERNIZATION OF INFRASTRUCTURE KUWA, ikitambulika kwamba mojawapo ya nguzo muhimu ya uchumi wa Kenya ni utoaji wa huduma za usafiri wa bahari; ikieleweka kuwa mataifa mengi hulazimika kutegemea bandari ya Mombasa ambayo hutoa huduma duni kutokana na kusambaratika kwa muundo msingi wa barabara na reli; ikitambulika kuwa mataifa husika kadhaa yanatafuta njia mbadala za kusafirisha bidhaa za nchi zao; ikizingatiwa kuwa huduma za reli zimedorora na kupelekea msongomano wa magari katika barabara zetu na kusababisha uharibifu wa barabara na ongezeko la ajali barabarani; bunge la Seneti linaihimiza Serikali ya kitaifa kuhakikisha kuwa taifa hili linaafikia ushindani wake kiuchumi kwa kuvipa kipao mbele upanuzi na uboreshaji wa bandari ya Mombasa, ujenzi wa reli inayotoka Mombasa hadi Uganda na ujenzi wa mradi wa LAPSSET."
}