GET /api/v0.1/hansard/entries/381790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381790/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Hoja hii ina uzito mwingi. Katika mchango wangu nitachukua msimamo wa Sen. G.G. Kariuki kuwa Hoja hii ifanyiwe mabadiliko ili ikubaliane na mahitaji ya Wakenya. Ningependa kusema mambo matatu juu ya Hoja hii. Jambo la kwanza ni kuwa mwito wa harambee ni mzuri sana katika nchi hii. Wanasiasa wengi hujihusisha na harambee katika maeneo yao kwa sababu wanataka kuwasaidia watu wao. Orodha yangu inaonyesha kutakuwa na harambee nyingi mwishoni wa wiki hii. Si lazima mimi nihudhurie harambee hizo zote. Viongozi waliochaguliwa katika Kaunti zao, si lazima wahudhurie harambee hizo zote kwa sababu wana mambo mengi wanayowafanyiwa watu wao. Kwa hivyo, harambee hutegemea mahitaji ya watu. Hakuna mwanasiasa ambaye hulazimishwa kuhudhuria na kuchanga katika harambee yoyote. Najua wanasiasa ambao hawajawahi kuchanga hela hata moja katika sehemu zao za uwakilishi lakini huchaguliwa wakati wa uchaguzi mkuu. Marehemu mhe. Martin Shikuku alikuwa mchungaji wa watu. Yeye hakuwahi kuchanga pesa katika harambee yoyote katika sehemu yake ya uwakilishi Bungeni. Tunapozungumza mambo ya harambee tunafaa kuelewa kwamba harambee huchukua mielekeo mitatu. Hii ndio sababu ninakubaliana na msimamo wa Sen. G.G. Kariuki kuhusu Hoja hii. Hakuna maana ya kumsaidia mtu halafu kumvua nguo baadaye kwa kutangaza shida zake na vile anavyoishi. Nimesimama hapa leo si kwa sababu nimechangia harambee nyingi lakini nilichaguliwa kwa njia halali. Hata hivyo, kuna watoto ambao nimewasomesha kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo kikuu. Watoto hawa hawakusomeshwa na Sen. Muthama ili wampigie kura. Hapana. Mimi nimesaidia taifa hili kwa sababu ninataka kuona watu wetu wamepata maarifa na ujuzi wa kuweza kukuza taifa hili. Tukifanya hivyo, watoto hawa watakapokuwa watu wazima hawatajihushisha na ukora na mambo mabaya kwa sababu watakuwa na ujuzi na maarifa ya kufanya kazi kihalali. Tunajua kuwa walimu wengi wa shule za msingi hapa nchini hawawezi kuwaelimisha watoto wao hadi vyuo vikuu. Hii ni kwa sababu pesa wanazopata hazitoshi. Leo wako barabarani wakidai nyongeza za mishahara yao. Ni huzuni kuwa wengi wao hawawezi kusomesha watoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}