GET /api/v0.1/hansard/entries/381792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 381792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/381792/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ingawa anafanya kazi. Zaidi ya asilimia 90 ya Wakenya ni watu wanaoishi katika hali ya umasikini. Huu ni umaskini ule wa chini kabisa. Kwa hivyo, tunapochanga pesa, huwa hatuchangi bure. Mimi sichangishi pesa ili watu wanipigie kura. Ningependa kupigiwa kura na watu ambao sijawasaidia ili mbele ya Mwenyezi Mungu, nisiwe nimebadilisha kazi ambayo ninafaa kuwa nikifanya ya kuwatumikia watu. Sitaki kuonekana kama ninatumia hongo. Sen. G.G.Kariuki alisema mambo haya yameleta ufisadi katika nchi. Pesa za harambee husaidia kulipa gharama ya matibabu katika hospitali. Tunaposema tuwe na kamati ya kuchunguza ni nani anayefaa kuchangiwa pesa, kweli tutapata jibu? Magonjwa mengi huwakumba watu. Unaweza kupata kuna mtu ambaye anafaa kupelekwa nchi ya India kwa matibabu. Hapo ndipo tunafanya harambee ya dharura ili tumsaidie mtu huyo kulingana na desturi za Kiafrika. Si kawaida ya sisi kutosaidia mgonjwa. Tusijifanye kwamba sisi ni wazungu. Ukienda kwa mzungu bila kumweleza kwamba utaenda kwake, hautapata chakula. Lakini unapoenda kwa Mwafrika, jambo la kwanza analofanya ni kukupikia chakula, chai au uji. Ukikataa kula, anahisi vibaya sana. Kwa hivyo, tunawachangia wagonjwa ambao hawajiwezi. Ni vigumu kupata Sen. G.G. Kariuki anaomba kuwa na harambee ili apate pesa za kwenda hospitali ya M.P Shah kwa siku mbili. Najua hawezi kufanya hivyo. Lakini kuna mtu ambaye amevunjika mguu ambaye anahitaji matibabu katika hospitali hiyo lakini hana pesa. Sisi huchangia pia matanga mtu anapokufa. Kuna msemo wa Kiafrika unaosema kuwa mtu hujizika akiwa hai. Kujizika ni kuungana na wenzako katika kijiji, kukusanya mapato na kusaidia katika kuwazika walioaga dunia. Harambee ya tatu ni ya elimu. Harambee hii hufanyika kuwasaidia watoto masikini. Wakati mwingi sisi huchangia shule ili wapate vifaa muhimu za masomo. Tunahitaji kuchanga pesa ili watoto hawa wasome na kuja hapa baadaye kama Sen. (Dr.) Zani. Ikiwa tutaondoa harambee hii na kusema inafaa kuchunguzwa, basi watoto wengi hawatasoma. Kuna pia harambee za makanisa. Kanisa ni msingi ambao tunajenga roho zetu na maisha yetu ya baadaye. Ingawa Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o ameleta Hoja nzuri ambayo itarekebisha mambo ya hongo na ufisadi, ninahimiza mabadiliko yafanyiwe Hoja hii ili tuwe na nafasi ya kujua ni akina nani wana haja zaidi ya kusaidiwa. Jambo hili halifai kufanywa kwa ujumla na kusema watu wachunguzwe. Umasikini wa mtu ni kipawa kutoka kwa Mungu na hata utajiri ni kipawa kutoka kwa Mungu. Uongozi ni kipawa kutoka kwa Mungu. Hata Bibilia inasema, waliopewa nyingi ni lazima watoe kwa wingi. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}