GET /api/v0.1/hansard/entries/382082/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382082,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382082/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kipchumba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 440,
"legal_name": "Onesimus Kipchumba Murkomen",
"slug": "kipchumba-murkomen"
},
"content": "Bi Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuunga mkono Hoja hii. Nimetiwa kiwewe na mawazo ya Sen. G. G. Kariuki, ya kwamba maovu yaliyofanyika katika miaka iliyopita yanaweza kuwa halali kwa sababu ilikuwa inaendeleza mafanikio ya wachache. Nadhani hizo ni fikira ambazo zinadunisha haki za watu. Kwa hivyo, ningependa tubadilishe ya kwamba maovu ambayo yameweza kufanywa wakati wowote na Serikali yoyote yaweze kupingwa na kukataliwa kwa enzi zote. Kwa hivyo, kuhusu Turkwel Gorge Dam, kwa wale ambao hawajui jina lake halikuwa Turkwel bali Tilkol. Tilkol ni jina la Kiturkana kusema kwamba mto unaweza kustahimili jangwa. Kwa kimombo wanasema; a river that withstandswilderness . Huo ndio ulikuwa mto wa kipekee ambao wakati wowote kukiwa na jangwa, mto huo ulibaki na maji. Hio ndio sehemu ambayo wananchi wa sehemu hiyo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}