GET /api/v0.1/hansard/entries/382084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382084,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382084/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "walitegemea. Turkwel Gorge ina tunnel ya kilomita saba. Na jambo ambalo linatisha sana ni kwamba wengi ambao tegemezi lao lililikuwa katika sehemu ile waliondolewa kutoka mashamba yao. Na sio pale peke yake bali ni sehemu nyingi. Kwa mfano, kule Baringo kuna mto wa Bosei ambako dam ilitengenezwa. Lakini baadaye wananchi hawangeweza kukitumia kidimbwi kile kwa sababu kilifungwa. Halafu pale chini ya mto hakuna nafasi na mtu akipatikana hapo anashtakiwa. Ninadhani hii ni Hoja nzuri kuweza kuhimiza Serikali kuona ya kwamba miradi yote ambayo iliweza kukuza maisha ya watu kwa njia isiyofaaa, wale watu wafidiwe, hasa sehemu ambazo maisha ya watu yamehatarishwa. Kwa mfano, pale Turkwel kuna mbu nyingi sana. Haifai kuwapatia watu wale mosquito nets peke yake kwani hizo zitawasaidia wakati wanapotembea? Nimesikia watapewa hata madawa ya kutibu malaria. Hiyo haitoshi. Inafaa watu wapewe sehemu nyingine ambako wanaweza kuendeleza maisha yao. Pia, kile kdimbwi ambacho kimekuwa kama bahari, wafunzwe mbinu za kuvua samaki na waelimishwe jinsi ya kupata soko la samaki. Watu wakiwachwa hivyo wanabaki maskini. Ninatilia maanani Hoja hii na kusema kwamba inafaa Serikali ihakikishe kwamba watu wanafidiwa. Inafaa watu wa Turkwel wajengewe shule, kwa maana ninaamini KenGen haijajenga shule yoyote pale. Kampuni hii inapeleka wapi faida ambayo inapata kutokana na mauzo ya nguvu za umeme? Inaonekana wakurugenzi ndio wanafaidika ilhali raia ambao maisha yao yamebadilishwa na mradi huu hawapati faida yoyote. Ninaunga mkono Hoja hii. Asante."
}