GET /api/v0.1/hansard/entries/382101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382101,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382101/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ninashukuru kwa nafasi hii ili nitume rambi rambi zangu na kilio changu kwa moyo wote kwa familia ya marehemu Njiru. Njiru alikuwa mwanasiasa aliyefaa na aliyestahili sana. Alichaguliwa kwa kuwaambia watu wake ya kwamba akichaguliwa atajishughulisha na majukumu ya kutatua shida za watu wa sehemu yake. Ninasikitika sana kwa sababu, bali na kuwa alipigiwa kura, alitaka kuwapa watu wake maji lakini aliwaacha bila maji. Alitaka wapate matibabu na hosapitali lakini aliwaacha bila. Baada ya miaka, 50, Njiru ameiacha nchi hii ikiwa sio vile alivyotaka. Lakini ninashukuru Mungu kwa kazi aliyofanya. Tunamtakia kila la heri katika maisha yake ya kwenda mbinguni. Mungu amuonee huruma na amuweke pahali pema peponi. Nasi tufanye kazi tukijua kwamba tutaondoka na tuna jukumu la kutoa huduma kwa watu wetu na kuona ya kwamba tunashughulikia nchi yetu iwezekanavyo. Naomba kutuma rambi rambi zangu."
}