GET /api/v0.1/hansard/entries/382140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382140,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382140/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Nyakeriga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13112,
        "legal_name": "Linet Kemunto Nyakeriga",
        "slug": "linet-kemunto-nyakeriga"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante sana kwa kunipa muda. Kwanza nashukuru daktari kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ni ya maana sana. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ukiangalia katika familia, utapata watu wanakosana kwa sababu ya kelele ambayo inasababishwa na dawa za kulevya na pombe harama. Maafa katika jamii yamezidi kwa sababu ya madawa ya kulevya. Utapata kwamba mtu akiwa safarini, anapewa tu peremende na kisha anaaga dunia na baadaye inapatikana kwamba alipewa madawa za kulevya. Bw. Spika, ukiangazia juu ya pombe haramu ya kumi kumi, utapata kwamba inafanya watu wengi kupoteza macho ama kuwa vipofu. Kwa upande mwingine, tunaona kwamba pombe na madawa ya kulevya yanaathiri sana uchumi kwa sababu pesa nyingi hutumika. Hii inaweza kuleta shida katika familia. Naomba kuunga mkono Hoja hii na kusema kwamba yafaa tuangamize madawa ya kulevya na pombe haramu."
}