GET /api/v0.1/hansard/entries/382238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382238/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangia Hoja hii. Pia ningetaka kuchukua nafasi hii kumshukuru Sen. Obure kwa kuleta Hoja hii inayowahusu wafanyakazi. Kama sote tunavyojua, mfanyakazi ni mtu muhimu sana katika uendelezaji wa uchumi wa nchi yetu. Lakini ni jambo la kusikitisha tukiona kwamba baada ya mfanyakazi kustaafu anapatikana barabarani, ofisini na nyumbani za marafiki akiomba omba ili apate namna ya kuweza kujikimu kimaisha. Ningetaka kuhimiza mapato ambayo yanapewa na mahakama yalipwe mara moja kwa sababu ni haki ya mfanyikazi. Mfanyakazi aliyefanya kazi au kwa bahati mbaya amepoteza kazi yake, ni sharti alipwe ikiwa mahakama imeamua alipwe. Ni jambo la The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}