GET /api/v0.1/hansard/entries/382240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382240/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kusikitisha kuona ya kwamba hata baada ya muda mrefu baada ya mahakma kupendekeza mfanyakazi alipwe kiasi fulani cha pesa bado anahangaika barabarani. Bi. Spika wa Muda, kwa upande wa wafanyakazi wanaofanya kazi katika makampuni ambapo kuna mitambo inayowaumiza mikono, miguu na sehemu zingine za mwili, waweze kulipwa bila taabu yoyote. Iwapo mfanyakazi aumie, asiweze kuendelea kufanya kazi tena, ni lazima afidiwe vilivyo. Ikiwa amejaza zile fomu na ni lazima alipwe, kuna umuhimu wa kuona ya kwamba huyu mfanyakazi amelipwa katika muda mfupi iwezekanavyo. Jambo la kusikitisha ni kwamba mara nyingi wale wafanyakazi wanapoumia katika kampuni wanabaki wakienda katika hayo makampuni kuomba ridhaa. Hatimaye mara nyingi wanaendelea kufanya hivyo mpaka mwisho wanafariki. Kunazo safari wanazofanya kutoka sehemu mbalimbali. Kwa mfano, kule Kaunti ya Kilifi, wakati nikifanya kazi kama hakimu katika korti ya viwanda, watu wengi walikuwa wakisafiri kutoka sehemu mbalimbali siku nzima ili wafike Nairobi. Hawa watu huwa wamestaafu ama wamewachishwa kazi ama wanafuata ridhaa ambazo zimepewa na korti. Hili ni jambo la kusikitisha. Wakifika hapa wanazungushwa katika ofisi mbalimbali. Hoja hii ni muhimu na itahakikisha kwamba malipo kama haya kama yamepeanwa, ni lazima yapelekwe kwa Serikali za mashinani. Wafanyakazi wengi wamekuwa wakipata taabu kuelimisha watoto wao. Mtu akifanya kazi na raha anaishi na familia yake vizuri. Mtu anapostaafu kwa kazi yake, malipo yake yanafaa kulipwa. Hayafai kuchelewishwa. Yakichelewa, watoto wanacha kwenda shule. Hoja hii ni muhimu. Tunafaa kuona malipo haya yamepelekwa mashinani. Bi. Spika wa Muda, jambo lingine ningependa kutaja ni kuhusu wazee ambao wamestaafu. Wakati unapofanya kazi, afya yako huwa nzuri lakini unapostaafu, haujiwezi tena. Ni jambo la kusikitisha kuona wakati ulipokuwa umeajiriwa kazi ni kama kuwa harusini, lakini wakati wa kuacha kazi unakuwa ni kama wakati wa mazishi. Hii ni kwa sababu unaanza kuhangaika na haujui maisha yatakavyokuwa. Ni haki yako kulipwa. Jambo hili linafaa kuchukuliwa hatua ili malipo yapelekwe mashinani. Hakuna haja ya mtu kutoka Kilifi Kaunti kuja Nairobi kufuata malipo yake. Hakuna haja ya mtu kutoka Kwale ama Mombasa na kusafiri usiku mzima kuja Nairobi kupata haki yake ambayo angeipata akiwa nyumbani. Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}