GET /api/v0.1/hansard/entries/382244/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382244,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382244/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ambaye anataka hayo yote anaweza kuwa ni masikini. Pengine anaweza kuwa amestaafu miaka kumi iliyopita na pengine hajapata malipo yake. Mtu huyu anahitaji kusafiri na malazi mema. Hayo yote ni masumbuko. Mtu huyu amenyimwa haki yake. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu Serikali inafaa kuchukua hatua na kuwalipa watu hawa mashinani. Tunafaa kuwa na njia mwafaka ambayo Wakenya wanaweza kutumia kupata haki yao. Watu hawa wameajiriwa na walikuwa wakilipwa, basi sioni kwa nini malipo yao ya uzeeni ichelewe kulipwa. Wakati huu hatutumii mfumo wa faili. Hapana. Tuko na mitambo ya tarakilishi. Mhe. Rais wa Kenya alisema hata mtoto wa mwaka mmoja atakuwa na tarakilishi mwaka ujao."
}