GET /api/v0.1/hansard/entries/382248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382248,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382248/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, hiyo ni sawa. Nikisema mwaka mmoja, namaanisha mtoto katika hali ya uchanga anaweza kuwa na tarakilishi. Kwa nini hapa Kenya hatuna mfumo wa kuweka faili za watu ambao wamestaafu na wanaohitaji manufaa mengine? Tunatakiwa kuwa na mbinu katika mashinani za kuwalipa watu wanapostaafu. Mtu akistaafu leo, kesho mambo yake yanafaa kuwa sawa kwa sababu watu ambao wanatuajiri wanajua ni nani amefikisha umri wa kustaafu. Haya yote ni mambo ambayo Wakenya wote wanafaa kuwaajibika. Wale wanaoajiriwa maofisini wanafaa kuajibika. Kuna wakati ambapo tulikuwa na maofisa ambao walikuwa hawajulikani lakini walikuwa wakilipwa na pia walikuwa katika orodha ya Serikali. Hayo yote yalifanyika kwa sababu ya kutowaajibika. Wakenya wote wanafaa kuwaajibika na mambo yafanyike vile yanavyopaswa kufanywa. Mambo hayafai kufanyika vingine. Tuwe na sheria ambazo zinatusaidia ili kila mmoja wetu apate haki zake wakati unaofaa. Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}