GET /api/v0.1/hansard/entries/382413/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382413,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382413/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Getrude",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, nafikiria Hoja hii inagusia sana maswala ya akina mama, mbali na visa vinavyozungumziwa kuhusu ujambazi pekee. Tunaona kwamba kuna umuhimu sana wa barabara hizi haswa inapofika wakati ambapo kina mama kule vitongojini wanapokuwa na uchungu wa kuzaa. Wengi wao hufa kwa sababu ya ukosefu wa barabara. Kwa hivyo, security roads zinaongelewa ni muhimu. Lakini barabara hizi zinahitajika kwa mambo mengi sana na sio tu kwa cattle rustling ama vita dhidi ya ujambazi. Kuna umuhimu wa barabara hizi kwa watu walio wagonjwa mahututi mahali hakuna barabara kama kwetu ninapotoka, Ugiriamani. Barabara tunazotumia ni hivi vibarabara vyembamba sana. Wakati mtu anapokuwa mgonjwa ni lazima abebwe na wheelbarrow. Ikiwa ni mama mja mzito wakati anapofika hospitali pengine amezalia njiani ama amekumbana na hatari zingine. Pia barabara hizi tunazozongumzia hapa zinalenga yule mhukumiwa kortini; watu ambao wako rumande kesi zao zinasikizwa. Kwetu tunapata kwamba kuna shida nyingi sana za mashahidi kufika kortini kwa sababu ya ukosefu wa usafiri. Kesi ambayo ingechukua miezi miwili inachukua hata miaka mitatu kwa sababu mashahidi wana kila sababu ya kutofika kortini kwa sababu hakuna usafiri wa kutosha. Kwa hivyo, barabara hizi zina umuhimu sana. Tukiangazia mambo yaliyotokea Baragoi wakati askari wetu waliuawa, kati yao, kulikuwa na kijana mmoja askari ambaye alifikiwa baada ya siku tatu. Kama barabara hizi zingekuwepo, kijana yule angeokolewa. Nikiongezea, naona kuna umuhimu wa simu ya dharura ya 999 kurudishwa. Pia, inafaa Serikali iwe na helikopta wakati ambapo tunaendelea kungoja barabara zitengenezwe. Wakati tulikuwa na 999, ilikuwai rahisi sana kuwasiliana na walinda usalama. Wakati huu tuko na laini ya safaricom na wakati wa hatari mpaka ukae uanze kufikiria namba kwa sababu sio rahisi kuijua kwa kichwa. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa Serikali kufikiria kurudisha simu ya dharura ya 999 na kuwa na heliktopta ya kushughulikia maswala ya dharura."
}