GET /api/v0.1/hansard/entries/382897/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 382897,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382897/?format=api",
"text_counter": 66,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa hii fursa. Ningependa kuchangia Hoja hii kwa kusema kuwa sisi watu wa mashinani mara nyingi huwa tunapata matatizo kutoka sehemu zingine. Kwa mfano, makampuni ambayo yako kwingine humwaga uchafu ambao unatuletea sisi shida. Jambo hili la pollution linaambatana na mambo mengine kama uharibifu wa misitu, unaofanywa na makampuni au mashirika ya Serikali. Mashirika haya huwa hayaangalii mathara wanayosababisha kwa watu. Bw. Naibu Spika, sisi watu wa Tana River tunapata mathara kila wakati kutokana na miradi ya kiholela inayoanzishwa na mashirika ya Serikali naya kibinafsi. Jambo hilo hutuletea Malaria na magonjwa mengine. Hivi majuzi nilikuwa nikilalamika juu ya TARDA na KenGen. KenGen hufungulia maji bila kutujulisha ili tuweze kujipanga. Maji haya hutuathiri, kutusomba na kutuletea magonjwa kila wakati. Kila wakati sisi watu wa Tana River tunaanzia mwanzo kwa sababu ya kupata hasara kutoka makampuni au mashirika ya kiserikali. Sababu inatakikana wakati jambo lolote likitaka kufanywa, lazima maslahi ya watu yaangaliwe kule mashinani na lazima watu wahusishwe wakati miradi inafanywa ili isiathiri watu. Kuna hizi polythene bags ambazo hutupwa kiholela na hivyo kuharibu mazingira na ilhali makampuni hayo huenda hata sio ya Wakenya. Tunasema kwamba ikiwa kampuni yoyote itakuwa mashinani, ni lazima walipe kiwango fulani ili waweze kupata fidia. Kwa hivyo, ninapongeza walioleta Hoja hii na ninaunga mkono bila tashwishi kwa sababu sisi tumechaguliwa kutoka kaunti na sisi ndio tunaathirika sana. Ningependa kusema kwamba kampuni za KenGen na TARDA ambazo zimekaa Tana River bila kupitia njia ya kihalali yafaa zilipe fidia na zituondokee kwa sababu tuna haja na ardhi hiyo. Tsavo West na Galana ziko katika eneo la Tana River. Wakaazi wa hapa walikuwa na ukosefu wa masomo lakini leo watu wa Tana River wanaelewa haki yao. Wale ambao walisema kwamba kutakuwa na project ya mamilioni ya irrigation ningependa kusema kwamba sehemu hiyo ni ya ufugaji na haitaweza kuwa mashamba. Sehemu hiyo tunaipangia kama watu Tana River. Watu wa Tana River wamezozania rasilmali kwa muda mrefu. Hii ndio sababu watu wanazozana kila wakati na wangependa kukaa chini na kujadiliana ni wapi watajenga na kufanyia miradi yao. Kwa hivyo, kila wakati ni lazima watu wahusishwe. Jambo la kutohusisha watu ndio chanzo cha mizozo na kuathiri watu kiafya na kiusalama. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}