GET /api/v0.1/hansard/entries/382904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382904,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382904/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "June 26, 2013 SENATE DEBATES 19 Sen. Boy Juma Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kunipatia nafasi hii nichangie Hoja hii muhimu sana. Kwanza, ninamshukuru aliyeleta Hoja hii na kumwambia kwamba siyo Murang’a, Embu, Kiambu, Machakos na Makueni pekee, hata sisi wapwani tumo. Kwa mfano, Kilifi na Malindi. Kwa hivyo, asifikirie tu kwamba kwake ndiko kuna shida, kwani mito hii inafika kule Pwani. Kwa hivyo mito hii ni rasilmali yetu Wakenya na rasilmali hii ndio sisi Wakenya tunajivunia. Nia na madhumuni ni kwamba mito hii ndio inatumika katika viwanda kwa sababu viwanda ndio maendeleo, viwanda vinabuni kazi na kukuza uchumi. Lakini viwanda hutoa uchafu. Hatukatai wananchi wapate kazi katika viwanda na tuwatoze ushuru, lakini kuna matokeo ya uchumi huu ambayo yanaharibu mazingira. Hilo ndilo lengo la Hoja hii. Ni kweli viwanda vinakuza uchumi, lakini kuna athari ya mwisho inayotokana na mazuri haya. Yule anayejenga kiwanda huwa amefanya utafiti na kujua mazao atakayoyapata, lakini Hoja inasema kwamba yule atakayeathariwa na maji machafu apatiwe manufaa fulani. Hii si siri wala ni ukweli wa mambo. Ni lazima mto uteremke chini, upende usipende. Hoja hii inapendelea kwamba wale wanaoathirika kule chini nao wapate faida inayotakana na manufaa ya viwanda. Bw. Naibu Spika, tukizungumza juu ya mito hii, kule kwetu Pwani upande wa Sabaki watu wanakunywa maji ya Mto Tana. Maji yanayotumika Mjini Mombasa yanatoka katika mito hii lakini ule uchafu unaotoka kwenye viwanda ni mwingi. Kuna mashirika mengi ya Serikali ambayo yamefanya vikao vingi na kuandika sera kuhusu mazingira; watu wanaenda Geneva, London na kwengineko lakini baada ya hivyo vikao, hakuna lolote linalotendeka. Kuna shirika kama NEMA, TARDA lakini hatuoni faida yao. Tunachoona wafanyakazi wakiendesha magari aina ya Prado. Hatuoni matokeo yoyote. Ndio maana kama Bunge la Seneti linalosimamia mambo ya kaunti kutoka juu hadi chini lihakikishe kwamba haki inatendeka. Ningependa kutoa mfano wa Mto Umba kutoka Kwale Kaunti ambao unatokea Tanzania kwenye Milima ya Usambara. Ndugu zetu Watanzania wameweka vidimbwi vya kutoa umeme. Ni tatizo gani linalotukumba sisi Wakenya? Mto wa Umba unapokauka, uchafu wote unaotokana na Mto Umba unateremka. Kila Desemba, pwani ya Lunga Lunga kuna Cholera kwa sababu maji huwa yameshuka katika mto. Pollution huwa juu. Watu hunywa maji ambayo yako polluted . Kiwango cha maji kutoka Lunga Lunga huwa chini. Inamaanisha kwamba watu wanakunywa maji machafu na ukinywa maji machafu unashikwa na Cholera . Chanzo cha Cholera ni Mto Umba. Maji yakishajaa, hatuna shida. Bw. Naibu Spika, kuna kiwanda kinachojengwa kule Ramisi na uchafu wake utaingia kwenye Mto Ramisi. Kule Marere, maji hayo yataingia kwenye mto huo. Uchafu wote wa kule Ukunda unaingia katika mito hiyo. Kule ndani kuna makaratasi na hata condoms. Ni lazima jambo lolote tutakalolizungumzia hapa litiliwe maanani. Ndio maana tukasema kwamba Sen. Muthama amefikiria jambo nzuri sana. Ndio maana nikasema kwamba, sisi kama Seneti, kuna haja ya kuhakikisha kwamba masilahi ya watu wetu wote yanalindwa. Isiwe tu kila wakati tunazungumza juu ya Budalangi kukiwa na mafuriko. Haya mambo hayasababishi yenyewe. Kuna sababu na inajulikana. Wakati utafika ambapo mvua itakuwa nyingi na mafuriko yatakuwepo. Mashirika haya ya kulinda mazingira hayafanyi kazi yake, ilhali yanapewa pesa kila mwaka. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}