GET /api/v0.1/hansard/entries/382906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382906/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ombi langu ni kwamba idara inayohusika– na ameelezea vizuri katika Hoja hii – itoe ripoti kila baada ya miezi sita na ifanyiwe kazi. Wakati umefika wananchi wanatarajia kufanyiwa kazi. Hii ndio maana tuko na Bunge la Seneti. Bunge la Seneti lipo hapa kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Haya mengi tunayozungumzia yameshazungumziwa kwenye Bunge na katika kongamano nyingi lakini mambo ni yale yale usiku kucha. Kwa hivyo, ni lazima kila mtu awajibike. Kama NEMA ama TARDA haziwajibiki, inafaa ijulikane. Haina haja kuwatwika wananchi mzigo. Hakuna haja ya kupatia watu kazi na magari makubwa ilhali wananchi hawapati huduma. Bw. Naibu Spika, uchumi wetu hautaendelea ikiwa kila siku tutakuwa tunatumia muda wetu kuwatibu kutokana na maradhi. Cancer imezidi na inasababishwa na kemikali zinazomwagwa kutoka kwa viwanda. Viwanda vinakuza uchumi, lakini athari zake ndio shida. Inafaa manufaa yake yawafikie wananchi. Kwa hayo machache, ninaunga mkono na ninamsifu Seneta ambaye amewasilisha Hoja hii."
}