GET /api/v0.1/hansard/entries/382929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 382929,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/382929/?format=api",
    "text_counter": 98,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Pia majuto ni mjukuu. Naunga mkono vile Hoja hii imerekebishwa na Prof. Lonyangapuo kwa sababu sisi katika Seneti tunajua kuwa kila Mkenya ni sawa na sehemu zote za Kenya ni sawa. Bw. Naibu Spika, ninafurahia Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. Muthama, akiwa na hekima. Tunataka kuipanua ili iangazie nchi nzima ili iwe na faida na kutoa mazao zaidi kwa nchi nzima. Hii ni kwa sababu tukiangaza mawazo yetu kwa nchi nzima, tunaona kuwa nchi nzima imeoza kwa uchafu na mipango mibaya ya binadamu. Imeoza pia kutokana na viwanda ambavyo vimestawishwa bila mipango. Imeoza pia kwa sababu desturi zetu za mazingara hazifai. Watu wanatupa kinyesi popote pale bila kujali. Imeoza kwa sababu sisi hatujali utu. Mazingira yakiwa mabaya mazingara huchafuka. Mazingira ni uhai na uhai ni mazingira. Kwa hivyo, ni lazima tutahadhari kabla ya hatari. Ni lazima turekebishe haya kabla utu na maisha tunayozingatia haijaangamia. Tunafaa kuangaza mawazo hata kwa sehemu za magharibi ambako kuna gugu maji. Ziwa Victoria linaangamia kwa sababu ya gugu maji. Hii ni kwa sababu watu walioko hawajatunza mazingira vizuri. Je, ziwa kama hilo likipotea na kuangamia ni sehemu kiasi gani ulimwenguni itaathirika? Maji hayo husambaa hadi nyanda za chini mpaka kaskazini mwa Afrika. Misiri, Sudan na nchi zingine zinatumia maji hayo na huku sisi tunayachafua. Haya ni mambo ambayo tunaweza kuyazuia. Juzi niliwaambia hapa kwamba Mkenya sasa hivi anatarajia kuishi kwa miaka 47 tu, ukilinganisha na miaka 70 na zaidi katika Uropa na kwingineko ulimwenguni. Inamaanisha kuwa katika Seneti hii wengi wetu hatufai kuishi tena kwa sababu tushapita kiwango hicho. Hii ni kwa sababu ya vitu vichache kama uchafuzi wa maji. Mwenzetu hapa alisema kuwa kila mnapoenda Pwani kujivinjari mnawacha kipindupindu. Mnafurahia lakini wale wanawachwa wakisaga meno na kuteta. Wanatumia pesa nyingi kusafisha uchafu huo. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, ni vizuri kuipanua Hoja hii na kuangaza mawazo yetu kwa nchi nzima ili Serikali iangaze kabisa fikira zake kwa mito yote katika nchi nzima, kisha itupatie ripoti mara mbili kila mwaka, wala sio mwaka huu, mwaka ujao au mtondogoo tu. Nafikiri kuwa jambo kama hilo litakuwa la manufaa na tutajua ni kiasi gani tutapiga hatua katika janga hili. Miswada na sheria kadhaa zishaangazwa katika Bunge tangu siku za zama. Kuna sheria ya mwaka wa 1999, kipengele cha 69. Hii sio sheria ya jana; sheria zipo. Mhe. Michuki alizitumia kusafisha Mto wa Nairobi. Kuna Michuki wangapi hapa? Kila wakati mhe. Michuki, basi, yeye kaanza basi na sisi tuendelee. Lazima tuyazoee hayo mawazo yake kwa sababu aliyawaacha kabla hajaenda zake, tuyatumie kuhakikisha kwamba mazingira ambayo tunaishi ni mazuri na mema. Yafaa tuhakikishe kwamba mazingira yametunzwa kwa dhati. Bw. Naibu Spika naomba kuunga marekebisho haya mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}