GET /api/v0.1/hansard/entries/383217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 383217,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/383217/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante sana, Bi Spika was Muda. Nchi yetu ni kama baba anayewala watoto wake halafu anaenda kwa jirani na kuchukua watoto wake na kudai ni watoto wake halali. Bi. Spika wa Muda, je, ni haki kwa Waziri wa Leba kusema Serikali ilidanganya walimu wakati fulani na sasa haiwezi kutekeleza yale yote iliyowaahidi? Ikiwa Serikali inawandanganya wananchi wake, basi Kenya imekwisha, hakuna pakwenda. Mimi ninaudhika sana ikiwa walimu hawatalipwa pesa zao. Ikiwa hakuna pesa, kwa nini Serikali inapendekeza kutenga Kshs700 miolini za kujenga ofisi na nyumba ya Rais aliyestaafu mwaka huu? Ninakumbuka Bunge la Kumi lilitenga kiasi fulani za pesa za kuwasaidia wakimbizi wa ndani wa kisiasa. Lakini pesa hizo hazikuwasaidia wakimbizi hao kwa sababu ya ufisadi Serikalini. Wengi wao wanaendelea kuishi katika mazingira duni na ya aibu. Bi. Spika wa Muda, Serikali inasema haina pesa za kuwalipa walimu na ilhali imetenga Kshs53 bilioni za kuwanunuliwa watoto wa darasa la kwanza tarakilishi kutoka China. Mwaka huu wakati wa uchaguzi, tuliletewa mitambo ya Biometric VoterRegistration (BVR) iliyogharimu Serikali pesa nyingi sana. Mitambo hiyo haikufanya kazi. Ilikuwa ni mitambo ya uongo. Serikali ilipoteza pesa nyingi sana ambazo zingetosha kuwalipa walimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}