GET /api/v0.1/hansard/entries/383776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 383776,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/383776/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda. Ningependa kuwashukuru waliozungumza mbele yangu na kuunga mkono mabadiliko yaliofanywa kwa sababu nchi ambayo haina historia haiwezi kustawi. Lazima tuangalie yaliopita ili tubadilishe historia kwa vizazi vijavyo. Bi Spika wa Muda, katika swala hili la watu ambao walifurushwa makwao, ni lazima tuangalie kwa historia. Watu wa Pwani walifurushwa kutoka kwao na Mwarabu na mpaka leo hawajawahi kupata ardhi yao kando ya bahari ya Kenya. Kwa hivyo, tukisema tuangalie tu ya sasa, basi tutakuwa tunasema kuwa tuponye mmoja na wengi waumie. Hiyo si haki au sheria ya Kenya. Kwa hivyo, naunga mkono turudi nyuma itakavyowezekana. Tatizo hili lilitokea hasa kuanzia mwaka wa 1992 kama tatizo la kisiasa, lakini tuwache siasa. Tusizingatie ni Wakenya wangapi walifurushwa makwao na makaazi yao na kuwekwa hohe hahe na kulala barabarani. Tukifuatilia hayo, basi mazungumzo haya hayatakuwa ya kisiasa bali ya kuboresha maisha ya Wakenya kwa kutatua matatizo haya. Bi Spika wa Muda, pili, tukianza kuangalia mambo ya kuboresha au kutatua matatizo na ardhi peke yake, nafikiri kuwa hiyo italeta vurumai. Unapozungumza mambo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}